Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge ameshinda mbio za Marathon za London kwa mara ya tatu mfululizo.

Kipchoge ambaye ni mmoja wa wakimbiaji hodari alianza mbio hizo akitumia muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 27.

Aidha, kwa upande wake mwanariadha wa Uingereza, Mo Farah yeye aliongoza katika hatua za awali kabla ya kupoteza mwelekeo na hivyo basi kumaliza nafasi ya tatu dakika tano nyuma ya Kipchoge.

Naye mwanariadha wa Ethiopia, Tola Shura Kitata aliweza kumaliza katika nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde 33 dhidi ya Kipchoge.

Hata hivyo, kwa upande wa wanawake, Vivian Cheruiyot wa Kenya alifanikiwa kudhibiti muda wake uliopelekea kufanya vizuri katika mashindano hayo.

 

 

Mohamed Salah ashinda tuzo za PFA
Baba Masogange ataja ahadi ya mwisho ya mwanaye