Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast na klabu ya Azam FC, Kipre Herman Tchetche amesema inatosha kucheza Tanzania na anahitaji kwenda kupata changamoto nyingine sehemu nyingine.

“Inatosha kwa muda ambao nimecheza Tanzania, nahitaji kuondoka kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine. Nimekuwa na maisha mazuri sana Azam, viongozi na wamiliki wanajali sana wachezaji, lakini nalazimika kuyaacha yote,”amesema.

Tchetche amesema kwamba hana mpango wa kuhamia klabu nyingine ya Tanzania na habari za yeye kuwa na mpango wa kwenda kwa mahasimu, Yanga ni uzushi.

“Nitoke Azam, niende Yanga? Usinifanye nicheke, mimi nimesema sitaki kuendelea kucheza Tanzania na hadi sasa sijasaini kokote hadi nipewe ruhusa na uongozi wa Azam,”amesema.

N'Golo Kante Azichimba Mkwara Arsenal, PSG
Gonzalo Higuain Amkataa Conte, Amkubali Klopp

Comments

comments