Klabu ya Azam FC imetoka kauli kuwa straika wao kutoka nchini Ivory Coast , Kipre Tchetche  yupo katika hatua za mwisho kuondoka klabuni hapo rasmi. Azam FC tayari wameonekana  kukubali  kumuachia mshambuliaji huyo  ambaye amekuwa katika mvutano na klabu hiyo.

Tchetche amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Azam FC lakini hajajiunga kambini huku kukiwa na taarifa kuwa anawaniwa na klabu kadhaa ikiwemo Young Africans.

Afisa habari wa Azam FC, Jaffary Iddy amesema kweli wapo katika mazungumzo na moja ya klabu nchini Oman kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo lakini kwa sasa hawezi kuitaja jina kwa kuwa bado mchakato unaendelea.

“Kuna klabu ya nchini Oman imeonyesha nia ya kutaka kumsajili Kipre, hivyo tunachosubiri kukamilika kwa mazungumzo na taratibu nyingine ili tumruhusu aondoke,”

“kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo akaondoka kutokana na suala leke lilipfikika, kwa hiyo tusubiri na kuona kama mambo yatakwenda kama yanavyotarajiwa na uongozi wa Azam FC.

Magari Ya Kutumia Umeme Yaanza Kufanya Kazi Nchini Kenya
Video: Koffi Olomide ampiga mnenguaji wake wa kike uwanja wa ndege