Jijini Nairobi mwanamke mmoja, Hannah Wanjiru anashikiliwa na polisi baada ya tuhuma za kutumia silaha ya panga kumkata mume wake Adrew Kamau sehemu za siri na kutokomea nazo.

Inasemekana kuwa mwanamke huyo alichukua uamuzi huo kwa kudai kuwa mume wake anamsengenya kwa wanawake wengine.

Kijana  huyo, Adrew Kamau sasa amelazwa katika hospitali ya Kijabe.

Kwa mujibu wa Kamau amesema kabla ya tukio hilo alipokea simu kutoka kwa mwanamke ambaye alitumia simu ya mkewe akidai ameiokota barabarani.

Lakini alipomaliza kuongea na simu hiyo ghafla mkewe ambaye alikuwa kando yake alidai kuwa mumewe alikuwa akimsengenya kwa mwanamke mwingine.

Hata hivyo Kamau alijaribu kumueleza mkewe kuwa alikuwa akizungumza na mwanamke aliyedai kuokota simu yake, lakini mwanamke huyo alipinga maelezo hayo.

‘’Alianza kunipiga hadi akaniangusha chini, lakini nilibaki nikimuonya kwa anachokifanya si sahihi, mara ghafla alinipigia na panga kichwani na kusababisha nipotezee fahamu. Alitumia mwanya huo kunikata sehemu zangu za siri kisha kutokomea nazo’’ amesema Kamau.

Baada ya kuzinduka kamau alipiga kelele kuomba msaada na kupelekwa katika hospitali ya kanisa  na baadae kupelekwa hospitali ya Kijabe.

Kaimu kamanda wa polisi, Stanley Mutungi amesema upelelezi unaendelea na ukikamilika mshitakiwa atapandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Video: Tumepata pigo kwa kuondokewa na mke wa Dkt. Mwakyembe-DC Hapi
Arsene Wenger: Narudia Tena, Sanchez Hauzwi