Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) amefarki dunia mara tu baada ya kutoa sadaka katika Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Mtaa wa Makanyagio B.
 
Mwenyekiti wa kigango hicho, Charles Kanyanda amesema Kangu ambaye ni mwanakwaya, alikuwa muumini wa Kanisa Katoliki, na Jumapili alihudhuria ibada ya Misa Takatifu ya asubuhi katika kigango hicho.
 
Amesema Beatrice alihudhuria ibada ya misa hiyo na kujiunga na mwanakwaya wenzake kama ilivyo kawaida yake akiwa kama mwanakwaya wa kigango hiko.
”Ibada ya Misa Takatifu iliendelea kama kawaida na ndipo ilipofika muda wa kutoa sadaka Beatrice alikwenda kutoa sadaka kama kawaida kisha akarudi kwenye nafasi yake na kuendelea kuimba ghafla baadaye alianguka na kupoteza fahamu”.
 
”Taharuki illibuka kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo ilipobainika kuwa alikuwa amekata roho” ameeleza Kayanda.
Watoto pacha walioungana kutenganishwa
 
Kanyanda alisema maziko yake yalifanyika katika makaburi ya Mwanga jana ambapo yaliongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Maria Imakulata, Monsinyori, Padri George Kisapa alielezea kuwa Beatrice alikuwa mcha Mungu na ameacha pigo kubwa kwenye kwaya ya Kigango cha Makanyagio B

Video: Wabunge waliotimuliwa CUF watinga mahakamani
Lukuvi atoa tahadhari kwa wakazi wa Dar dhidi ya matapeli