Polisi huko Italia katika mji wa San Donato wamewaokoa watoto 51 wote wakiwa salama waliokuwa wametekwa na dereva wa basi lao la shule ambaye alimwagia petrol na kulichoma moto basi hilo likiwa na wanafunzi hao wa shule ya Vailati di Crema iliyo karibu na jiji la Milan.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na watoto hao walionusurika, wamesema kuwa dereva wao alikuwa anataka kuwaua kwa kulipiza kisasi baada ya kupoteza watoto wake watatu waliouawa katika tukio la mauaji ya wahamiaji yaliyofanyika katika bahari ya Mediterranean.

Hata hivyo msemaji wa polisi Marco Palmieri amesema kuwa mara baada ya kumtia pingu mtuhumiwa huyo wa mateka alipiga kelele kwa nguvu akisema ”Acheni mauaji huko baharini, nitaangamiza watu wengi”

Aidha baadhi ya watoto walipata nafasi ya kuelezea namna walivyoweza kutoa taarifa polisi wakiwa ndani ya basi hilo na kueleza kuwa;.

”Tulikuwa tunaogopa, alitufunga mikono na kuzima simu zetu tusiweze kuwapigia polisi, lakini mmoja wetu simu yake ilianguka na hakufanikiwa kuiona, ndiyo ilitumika kuwapigia simu polisi’

Watoto wote waliokolewa wakiwa salama bila majeruhi yeyote ambapo polisi walifungua kwa nguvu mlango wa nyuma wa gari hilo na kuokoa watoto wote huku dereva wa gari hilo akitishia kujiua.

Serikali ya Itali imeifungia bandari yake kutoa misaada kwenye meli zinazochukua wahamiaji kutoka fukwe za Libya.

Kwa taarifa iliyotolewa na umoja wa mataifa umeonyesha rekodi ya zaidi ya wakimbizi 2,297 hupotea kwenye bahari ya Mediteranean wakijaribu kuingia bara la ulaya.

Habari Picha: JPM akutana na Naibu waziri mkuu wa Qatar
CHADEMA haijapoteza mvuto- Dkt. Mashinji