Afisa Habari wa Young Africans Hassan Bumbuli amesema Iwe Isiwe klabu hiyo itamsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Benard Morrison, licha ya Uongozi wa Simba SC kumbania kumpatia Barua ya Kumuachia (Release Letter).

Simba SC imeshaweka wazi mpango wa kutoa Barua ya kumuachia Morrison, kwa kuitaka Klabu inayotaka kumsajili kuwasilisha Barua ya kutaka kumsajili, ili taratibu nyingine ziendelee.

Bumbuli amesema Young Africans imejiandaa kwa mambo mengi na makubwa kuelekea msimu ujao, na amewakikishia Simba SC kupitia maumivu mara mbili, kama ilivyokua kwao kwa misimu minne iliyopita.

Amesema wanashangazwa na Simba SC kugoma kumpa Barua ya kumuachia Morrison, ili hali walishampa mkono wa kwaheri kwa kuandika Barua ya wazi kwa wadau wa soka Tanzania, lakini amesisitiza kuwa mchezaji huyo atacheza Young Africans msimu ujao.

“Mmekwisha, mnamtakia mchezaji kila la kheri katika maisha mapya. Sijui mmempa likizo mpaka mwisho wa msimu, Sasa nasema hivi, maumivu tuliyoyapitia sisi, wao watayapata mara mbili, acha waendelee kung’ang’ania”

“Atacheza Young Africans msimu ujao, Iwe Isiwe, tumejipanga kwa mambo mengi na makubwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa,” amesema Bumbuli

Kauli hiyo ya Bumbuli inadhihirisha hitaji la Young Africans kwa Morrison kuelekea msimu ujao, licha ya klabu hiyo kuendelea kufichwa katika sakata la mchezaji huyo kuondoka Simba SC.

Majaliwa ateta na wanaohama kwa hiari Ngorongoro
FC Barcelona kuhamia Lluis Companys Olympic Stadium (Montjuic)