Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Serikali ya Marekani, John Kirby amesema tukio la Ndege ya kijeshi ya Urusi, kugongana na ile ya Marekani isiyokuwa na rubani na kuanguka katika Bahari nyeusi, linatafakarisha kwakuwa Bahari nyeusi ni ya wote.

Jeshi la Marekani, limethibitisha kuanguka kwa ndege yake wakati ikifanya doria katika anga la kimataifa, ikiishtumu Urusi kwa kuilenga ndege yake huku Brigedia Jenerali Patrick Ryder ambaye ni msemaji wa Wizara ya Ulinzi nchini Marekani akisema kitendo hicho si cvha kitaalam.

Amesema, “Tulichokiona ni kwamba ndege ya kijeshi ilirusha mafuta mbele ya ndege yetu isiyokuwa na rubani na hivyo ikaharibu ubavu wake mmoja.” huku Balozi wa Urusi nchini Marekani, Anatoly Antonov, akisema jeshi la nchi yake lilichukua tahadhari ya kiusalama.

“Ndege hii isiyokuwa na rubani inaweza kubeba tani Elfu Moja mia saba za vilipuzi na mabomu, Je Marekani ingefanyaje iwapo ingeona ndege ya Urusi karibu na New York?” alihoji Anatoly Antonov katika tukio linalohatarisha uwezekano wa Marekani kukabiliana na Urusi, kutokana na vita vya Ukraine.

Meridianbet yawapatia Reflectors Bodaboda
Maboresho Bima ya Afya: NHIF yatoa ufafanuzi