Siku chache zilizopita wasanii wa bongo wameshika kasi sana kwa kutoa video za nyimbo zao mpya ambazo zinafanya vizuri sana kwenye chati ya muziki Youtube.
 
Leo tuwaangalie wanamuziki watatu walioachia video zao siku moja, July 10 2017,  Diamond Platinum ‘Eneka’, Vanessa Mdee ‘kisela’ pamoja na mwanadada anayekuja kwa kasi sana katika tasnia hii Nandy ‘Wasikudanganye’.
 
Kisela ni muziki mzuri sana uliotengenezwa na mwanadada Vanessa Mdee akishirikiana na mashuhuri wakongwe wa muziki mapacha toka Nigeria maarufu kama Psquare, kwa sasa video hiyo imekwisha tazamwa na watu 281,251, kwa mantiki hiyo ni video inayoongoza kwa kuwa na watazamaji wengi kulinganisha na video ya Eneka na wasikudanganye.
 
Eneka ni wimbo ulioandikwa na Diamond mwenyewe na mdundo wake kutengenezwa na Laizer Classic kutoka Wasafi Records, video ilichukuliwa nchini South Africa na muongozaji akiwa Director Seasan, kwa sasa video ya Eneka  imeshatazamwa na watu 270,911.
Nandy akiwa nyuma anawafukuzia wakongwe hao kimuziki na video yake ikiwa bado inaendelea kufanya vizuri na tayari imekwisha tazamwa na watu zaidi ya 165,681 ambayo ni matokeo mazuri kwa msanii ambaye juzi tu ndio ameingia kwenye sanaa hii.
 
Ushindani bado ni mkubwa sana, Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram ametupia post akionesha video yake kali inakuja akiwa amemshirikisha Patoranking, Video hiyo inatarajiwa kuachiwa Sept 1, mwaka huu.
 
Huku Alikiba nae akiwa amewaandaa vyema mashabiki wake kwa post za instagram kusubilia kichupa chake na msanii toka Nigeria Davido.

Aubameyang aweka wazi hisia zake kwa klabu ya Chelsea
Majaliwa akabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa Ruangwa