Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo.


Akizungumza baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo, Martin Ngoga katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao akiwa mkoani Dar es Salaam, Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Dkt. Mpango awapa kazi Wizara ya Mambo ya Nje

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.


“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” amesema Balozi Mulamula.

Young Africans yampotezea Kibu Denis
Dkt. Mpango awapa kazi Wizara ya Mambo ya Nje