Wizara ya afya Zanzibar imezindua zoezi la siku kumi la kupulizia dawa ya kuulia viluilui vya malaria majumbani ambalo limeanza februari 13 hadi februari 21

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo Naibu Waziri wa afya Said Suleiman amesema zoezi hilo litazihusu shehia 76 Unguja na Pemba

Suleiman amesema baadhi ya shehia katika wilaya zote za unguja zitapuliziwa dawa na Pemba ni wilaya ya mkoa yenye shehia moja wenye shehia tano na Micheweni shehia tatu ambapo wilaya ya Unguja imebainika kuwa na maambukuzi ya malaria kuliko wilaya ya Pemba hatua iliyolazimu shehia nyingi kupuliziwa dawa.

Aidha amewataka wananchi watakao puliziwa nyumba zao dawa kutoa ushirikiano kwa wapiga dawa ikiwa ni pamoja na kuandaa makazi yao na kutayarisha maji yatakayotumika kwa kazi hiyo.

Hata hivyo amewatoa wasiwasi wananchi kuwa vijana watakao fanya kazi hiyo wamepewa mafunzo maalumu ya uadilifu na hivyo wasiwe na mashaka nao.

Naye mkurugenzi wa elimu ya afya dkt.Fadhil Abdalah amesema zoezi la kupulizia dawa majumbani ni moja ya mikakati inayotumiwa na wizara hiyo katika kupambana na Malaria.

Ameongeza kuwa kiwango cha malaria Zanzibar bado kipo chini ya asilimia moja lakini lengo la wizara ni kuhakikisha maradhi hayo yanamalizika kabisa.

Matusi yamng’oa Mbunge wa Ndanda CHADEMA, aomba nafasi tena CCM
Serikali yataja sababu kuzuia wanafunzi wa China kurejea nchini