Baraza la Kiswahili Tanzania – BAKITA, limeendesha darasa la kwanza la Kiswahili kwa walimu 49 nchini Malawi mwezi Novemba, 2022 na walimu 38 nchini Burundi mwezi Desemba, 2022.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi chana ameyasema hayo jijini Dodoma na kkuongeza kuwa mafunzo hayo yamejenga hamasa kubwa na kusababisha walimu wa Kiswahili katika nchi hizo kuhitaji mwendelezo wa mafunzo hayo.

Amesema, kutokana na vuguvugu hilo, walimu wa Burundi wameanza harakati za kuundwa kwa baraza litakalosimamia maendeleo ya Kiswahili nchini humo kutokana na hamasa waliyoipata.

Aidha, amesema pia BAKITA lilishirikiana na ubalozi wa Nigeria kufanikisha darasa la Kiswahili la Waandishi wa Habari 27 wa Voice of Nigeria (VON) mwishomi mwa mwezi Mei, 2023.

Dkt. Chuachua ataja kusudio uanzishwaji mradi hifadhi ya misitu
Waliowateka wafugaji 30 waandika barua kutaka fidia