Ile subira ya muda mrefu ya Watanzania juu ya matumizi ya Kiswahili Kama lugha rasmi SADC, hatimaye imevuta heri, Kiswahili kimetangazwa kuwa lugha rasmi ya nne ya jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC, Dk, Hage Geingob, ndiye aliyetangaza lugha hiyo kutumika rasmi SADC Jana, alipokuwa anahutubia mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa jumuiya hiyo kabla ya kukabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya, Rais wa Tanzania, Dk, John Magufuli.

“Natangaza rasmi kwamba Kiswahili kitakuwa lugha rasmi ya nne ya SADC” alisema Dk, Geingob ambaye Ni Rais wa Namibia.

Hatua hii inawezesha Kiswahili kutumika katika shughuli rasmi za jumuiya ambapo kitatumika sambamba na lugha nyingine rasmi za SADC ambazo ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa.

Kwa upande wa waliohudhuria Mkutano huo, viongozi kutoka Nchi 16 za Afrika, walilishangilia kwa shangwe na kusimama, kuonesha kuunga mkono na kupendezwa na tangazo hilo.

Awali Rais Magufuli alipotoa hotuba ya makaribisho, alieleza kuwa Kiswahili ni lugha ya 10 duniani kuzungumzwa na watu wengi, ni lugha rasmi umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pia ni lugha rasmi kwa Benki ya maendeleo ya Afrika ( AfDB).

Sambamba na hayo, baadhi ya Marais waliongea maneno ya Kiswahili katika Mkutano huo wa SADC jana, ambao ni Rais wa Comoro, Azali Assoumani, Rais wa Namibia Dk, Geingob, Rais wa DRC Felix Tshisekedi na Rais wa Tanzania Dk, John Magufuli.

 

 

Video: Kasi ya maendeleo ya JPM yahamia SADC, Ajali ya Moro ilivyorejesha machungu ya mwaka 2000
Waliokatwa mikia CCM wajitembeza Lumumba