Shirikisho la soka barani Afrika CAF hii leo litaendesha zoezi la upangaji wa makundi ya fainali za bara hilo za mwaka 2017, katika hafla maalum itakayofanyika mjini Libreville nchini Gabon.

CAF wataendsesha zoezi hilo baada ya mataifa 16 yatakayoshiriki fainali hizo kufahamika tangu mwezi uliopita.

Hata hivyo CAF watatumia vigezo vya ubora wa timu zilizofuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2017 kupangwa katika makundi manne tofauti.

Katika upangaji huo wa makundi chungu cha kwanza (Pot 1) kutakuwa na wenyeji Gabon, mabingwa watetezi Ivory Coast, Ghana pamoja na Algeria.

Mataifa hayo yatakuwa vinara wa kila kundi, na kisha yataunganishwa na mataifa mengine ambayo yamewekwa katika vyungu namba mbili hadi nne (Pots 2-4). ambapo mataifa haya ndio yataunda manne ya ushindani.

Chungu cha Pili (Pot 2): Tunisia, Mali, Burkina Faso, DR Congo

Chungu cha Tatu (Pot 3): Cameroon, Senegal, Morocco, Egypt

Chungu cha Nne (Pot 4): Togo, Uganda, Zimbabwe, Guinea Bissau

Masauni afanya mazungumzo na wajumbe kutoka UNDP
EFA: Mashabiki Wa Misri Ruhsa Kuingia Borg El Arab