Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetakiwa kuhakikisha kuwa wananchi wake wanatumia mavazi ya kiafrika hususan kitenge kama vazi rasmi la kiofisi badala ya suti.

Akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya baraza hilo yaliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, Mkurugenzi Mtendaji wa baraza hilo, Lilian Awinja alisema kuwa wananchi wa Afrika Mashariki wanapaswa kuacha kuvaa mavazi yanayoingizwa kutoka Ulaya na Marekani ambayo mengi yanakuwa yametumika, badala yake wavae mavazi mapya na yanayowakilisha uafrika.

“Kwanini Waafrika wavae nguo zilizotumika kama nguo za ndani na hata suti wakati tuna Vitenge vyetu?” Awinja alihoji. “Tunawaomba viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya kitenge kuwa vazi rasmi la kiofisi hasa siku za Ijumaa. Wananchi wao waende ofisini na vazi la kitenge,” aliongeza.

Hata hivyo, alisema kuwa hawaombi kuzuia mavazi yanayotoka Ulaya na Marekani lakini anasisitiza Waafrika kupewa nafasi ya kufurahia mavazi yenye utambulisho wao kwa vitendo.

Alisema hata Rais Museveni hivi sasa anavaa kitenge kama vazi rasmi la kiofisi badala ya suti na kwamba hiyo ni njia sahihi ya kulipa umaarufu vazi la kitenge.

Msemaji wa Serikali atolea tamko waraka wa baraza la KKKT
Njombe Mji FC warejea TFF, Bodi ya ligi