Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo jana tarehe 5 Mei 2018 alifika katika Kijiji cha Tundu, Kata ya Kidodi kutekeleza agizo la Rais Magufuli.

Hatua hiyo ni kufuatia simu iliyopigwa na Rais Magufuli akimtaka Prof. Mkumbo kutatua kero ya maji katika eneo la Kidodi inayowakabili wananchi wa mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo katika ziara hiyo Rais Magufuli mkoani humo aliagiza kukamatwa kwa Mkandarasi wa Maji Kata ya Kidodi, Morogoro kwa kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Bodi ya mikopo kuanza kupokea maombi mwezi huu
Furahia wikendi yako na video hii kutoka kwa Ngoma wa Cameroon