Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema idadi ya wagonjwa wa kifafa nchini inakadiriwa kuwa millioni moja ambapo wanaoishi na tatizo hilo wako katika hatari ya kupoteza maisha mara sita zaidi ukilanganisha na jamii kwa ujumla wakiwemo vijana wenye umri wa wastani wa miaka 15.

Daktari bingwa wa ubongo, Uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kutoka katika hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk patience Njenje amesema ulaji wa nyama ya nguruwe ambazo hazijaivishwa vizuri umekuwa ukisababisha ongezeko la ugonjwa wa kifafa.

Dk Njeje amesema hatari ya ulaji wa nyama hizo inatokana na wanyama hao kuwa na minyoo aina ya Tengu ambayo inauwezo wa kusababisha uvimbe kwenye ubongo.

‘’Sababu za kifafa zipo nyingi ajali inachangia kwa asilimia 10 mpaka 15 ya wagonjwa nchini ongezeko linakuja kutokana na ongezeko la usafiri wa bodaboda ambapo ajali inapotokea mtu huweza kuumia kichwa na ukiumia kinachofuatia ni ubongo kuwa na kovu hivyo huko mbeleni unaweza kuwa na kifafa’’ amesema Dk Njenje.

Amesema kuwa utafiti uliofanyika hapa nchi unaonyesha katika kila watu 1000 watu 37 wana tatizo la kifafa huku zaidi ya watu milioni 60 wakikumbwa na tatizo hilo duniani.

‘’Kwa kila mwaka kunaongezeko la watu 70 kati ya 100,000 duniani kote hivyo kidunia ugonjwa huu una kasi kubwa hasa kwa upande wa Afrika ugonjwa huu uko mbele mno ambapo kila watu 1000 watu 50 wameathirika na kifafa asilimia kubwa wanatoka Afrika .

Tafiti zilizofanyika Mahenge, Morogoro za ugonjwa wa kifafa kwa Afrika Tanzania inaongoza wagonjwa, wanahatari ya kufa mara sita zaidi ya mtu ambaye hana kifafa alisema Dk njenje

Amesema kuwa asilimia 36 ya jamii wana imani potofu kuhusu ugonjwa huo hali ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutofika hospitali kwa wakati..

 

 

Idadi ya Wamarekani waliojeruhiwa kwenye shambulizi la Iran yapaa, Trump atoa tamko
Kinana, Makamba wakubali yaishe, Warioba aibuka tena Katiba Mpya

Comments

comments