Mchekeshaji maarufu nchini Afrika Kusini amefanya tukio lilipata umaarufu mkubwa nchini humo baada ya kueleza mkasa unaotoa picha kuwa yeye ndiye mama yake mzazi Beyonce.

Mchekeshaji huyo, Thenjiwe Moseley akiwa katika harakati za kuaminisha watu na kujiingizia kipato kwa kazi yake, alidai kuwa alikuwa anafanya kazi katika hotel ya kitalii jijini Durban mwaka 1984 na aliamua kumgawa Beyonce baada ya kutokea machafuko katika jiji hilo.

Amedai kuwa ilimchukua muda mrefu bila kumuona hadi aliposhtuka kumuona kwenye TV.

Amedai kuwa jina halisi la Beyonce ni Busisiwe na amemtaka arudi Afrika Kusini na mumewe Jay Z ili wafanye matambiko ya kumkaribisha nyumbani baada ya miaka mingi.

Ukawa wawapooza waathirika wa ‘Bomoabomoa’
Korea Kaskazini yajiandaa kufyatua bomu la nyukilia, Kusini yajipanga kujilinda