Maafisa kadha wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kituo cha polisi eneo la Kapenguria, kaskazini magharibi mwa Kenya.

Mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwakuhusika katika ugaidi,

Inasemekana upo uwezekano kuwa maafisa watano wa polisi wameuawa gazeti la Daily Nation limeripoti.

Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa kutokana na ushambuliwaji uliofanywa huku ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema polisi zaidi wameagizwa eneo hilo tovuti ya Capital Fm kilimnukuu.

CB66YqHWIAA_To7

“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anashikiwa alichukua  bunduki na kuanza kufyatua risasi,” Bw Boinnet amenukuliwa.

Hata hivyo Kituo hicho sasa kimezingirwa na juhudi za kukabiliana mshambuliaji zinaendelea.

BBC

Zlatan Ibrahimovic Kuachwa Safari Ya China
Adidas Waipandisha Man Utd Viwango Vya Utajiri Dunaini