Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ameendeelea kukosoa ununuzi wa ndege mbili za Bombadier Q400 ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kutetea maamuzi hayo.

Kitwanga amewatupia lawama watendaji wa Shirila la Ndege la ATCL akidai kuwa ndio walishauri vibaya na kusababisha kasoro katika manunuzi hayo.

Kitwanga

Mbunge huyo wa Misungwi, amesema anamuunga mkono Rais John Magufuli kwa asilimia 100 kwa uamuzi wake wa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 500 kununua ndege, lakini watendaji wa ATCL walishauri vibaya na kuchukua uamuzi wa kununua ndege hizo mbili zinatumia injini ya mapanga boi badala ya jeti.

“Mheshimiwa Rais ametoa hela tu. Watendaji wanasema walishindanisha kampuni mbili, lakini kwa mkakati upi?” Kitwanga aliliambia Nipashe.

“Ndege ulizonunua zinaendana na mipango yako? Tatizo hatuna mipango,” aliongeza.

Ingawa Serikali ilieleza kuwa ilinunua ndege hizo ili kuendana na hali ya mazingira ya nchi na gharama za uendeshaji kwani zinaweza kutua kwenye viwanja vingi zaidi nchini, Kitwanga amesema kuwa ndege hizo zinaweza kushindwa katika ushindani na makampuni yenye ndege zinazotumia injini ya jeti katika safari za ndani.

“Kwa sababu mna shilingi bilioni 500 kwenye bajeti, tulipaswa kuangalia ndege za kununua kwa ajili ya njia za Kigoma, Tabora… Mwanza na Kilimanjaro,” Kitwanga anakaririwa.

Alisema kuwa kabla ya kuagiza ndege hizo, serikali ilipaswa kusoma ndege zinazotumiwa na washindani ndani ya nchi, na kwamba kiasi cha fedha kilichotolewa na Rais kingeweza kutumika kununua kwa awamu ndege zinazotumia injini ya jeti kwa awamu.

Mtaka Yote Hukosa Yote, Ndoa Ya Stand Utd Na Acacia Yavunjika
video: Naibu waziri atoa wito kwa wanasiasa na wananchi kutokushiriki maandamano yeyote