Kiumbe mmoja wa ajabu aliyepigwa risasi na mkulima huko Montana nchini Marekani amewashangaza Wataalamu nchini humo baada ya kushindwa kutambua familia yake huku wakimfananisha na Mbwa Mwitu.

Mkulima huyo amesema kuwa alimpiga risasi kiumbe huyo mara baada ya kuwasogelea mifugo wake akihofia kuwadhuru.

Wataalamu wa wanyama pori wamesema kuwa wameshindwa kutambua ni familia ipi ya wanyama anayotoka kiumbe huyo.

Aidha, baada ya kumchunguza kiumbe huyo wamesema kuwa huenda akawa ni Mbwa Mwitu kwa sababu meno yake ni mafupi na makucha ni marefu sana.

“Hatujafahamu hasa huyu mnyama ni wa familia ipi hadi uchunguzi wa DNA ukamilike ndipo tutakapo toa jibu sahihi,”amesema Msemaji wa shirika la samaki na wanyamapori.

Hata hivyo, amesema kuwa uchunguzi unaofanywa kwa njia ya DNA utachukua wiki moja ili kuweza kutoa jibu sahihi la mnyama huyo.

 

 

Zaidi ya watu 100,000 huumwa na nyoka, WHO yapitisha azimio
Makala: Wimbo wa Mpoto ulihitaji kiki ya uongo ya MC Pilipili na ..?