Baada ya Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans, Fiston Kalala Mayele kushinda tuzo ya Kiatu cha Dhahabu ya mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika akiwa na mabao saba, kiungo wa AS Real Bamako ya nchini Mali Ibrahim Sidibe amesifu uwezo wa Mshambuliaji huyo.

Mayele aliifunga Bamako nje ndani wakati timu hizo zilipokutana Kundi D la Shirikisho na kule Mali alifunga moja katika sare ya 1-1, na kisha akawafunga jingine moja Dar es Salaam, Young Africans ikishinda 2-0.

Kiungo wa AS Real Bamako Ibrahim Sidibe

Bao jingine la Young Africans lilifungwa na Jesus Moloko, huku Yanick Bangala akikosa Penati katika dakika ya 68.

Sidibe, ambaye timu yake ilishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama tano Kundi D huku Young Africans ikimaliza kinara kwa alama 13, amesema Mayele sio mtu wa mchezo.

“Wachezaji wote wa Young Africans wamefanya vizuri msimu huu lakini katika mafanikio yao huwezi kuacha jina la mtu kama Mayele kwa sababu katika michezo mingi na migumu aliiamua yeye hivyo kwangu nampa pongezi,” amesema Sidibe

Aidha, Sidibe ameongeza kwa alichofanya Mayele ni dhahir timu nyingi kubwa zitamuhitaji hivyo ni jukumu la viongozi wao kuhakikisha wanamboreshea mkataba wake ili aendelee kusalia kwenye timu.

TPA yafafanua minong'ono uuzwaji Bandari ya Dsm Dubai
Ma' RC simamieni Elimu ya haki, ulinzi wa Wazee - Gwajima