Kivuko cha MV. Nyerere ambacho kinafanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukara Wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza kwenye Ziwa Victoria kimezama, huku idadi ya watu waliokuwa kwenye kivuko hicho bado haijajulikana.

Kwa mujibu wa taarifa kufuatia tukio hilo, bado shughuli ya uokozi inaendelea, ambapo Serikali kupitia Wizara yake ya Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano (TAMESA) imewaomba wananchi wote kuwa na subira wakati taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la kusikitisha zikiendelea kutolewa.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 21, 2018
Breaking News: Madereva 50 wa Uber wanyang'anywa magari

Comments

comments