Vatican imesema kuwa inachunguza tukio la akaunti rasmi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani (Papa) ku-like picha ya mrembo aliyevaa nguo zisizo za staha.

Katika hali isiyo ya kawaida, ilionekana akaunti hiyo ya Papa ili-like picha ya mrembo wa Brazil, Natalia Garibotto. Bado haijafahamika ni lini hasa akaunti hiyo ili-like picha hiyo na nani hasa alihusika.

Taarifa ya tukio hilo ilianza kuripotiwa na vyombo vya habari Ijumaa iliyopita ikiwa na ‘screenshot’ inayoonesha ‘like’ hiyo, lakini wakati huo tayari ilikuwa imeshaondolewa (yaani ime-unlike).

Idara maalum katika Ofisi ya Papa inayoshughulika na vyombo vya habari imeiambia BBC kuwa wanachofahamu ‘like’ hiyo haikufanywa kwa namna yoyote na Ofisi ya Papa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uongozi wa Vatican unafanya kazi na Instagram kuona hiyo like ilitokea wapi.

Akaunti rasmi ya Instagram ya Papa ambayo inatumia jina la ‘franciscus’ ina wafuasi zaidi ya 7.4 milioni duniani kote.

Vyanzo kutoka Vatican vililiambia gazeti moja la Kikatoliki kuwa akaunti hiyo inasimamiwa na timu ya watu walioajiriwa na kwamba uchunguzi wa ndani pia unaendelea kubaini kama kuna mmoja kati ya watu wa timu hiyo alihusika.  

Katika hatua nyingine, Garibotto, mrembo mwenye mambo mengi kwenye mtandaoni, yeye amedai kuwa alifurahi kuona ‘like’ hiyo.

Alitweet, “angalau sasa nina uhakika naenda mbinguni.”

Prof. Kabudi : Hatutakubali Kudhalilishwa
Haya hutokea unapotumia manjano katika chakula