Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited  kilichopo  mjini Mtwara kusini mwa Tanzania,  kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.

Kwa Mujibu  wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.

Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.

Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa  utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.

Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Video: 'Hawatapenya mbele ya Serikali yangu' - Magufuli
Polisi Yakamata Vinara Wawili Wezi Wa Magari Jijini Dar es salaam