Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla, amegundua Kiwanda feki cha kutengenezea  Konyagi, Smirnoff feki na bidhaa zake kwenye nyumba ya mwanamke aliyejulikana kwa jina la Koku na maarufu kama Mama Kareem eneo la Sinza Kijiweni, Dar es salaam.

Tukio hilo limetokea Novemba 15, 2016 baada ya Naibu Waziri huyo aliyeongozana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama kuvamia kiwanda hicho na kukamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu pamoja na spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo na vifungashio.

pombe-feki5

Kiwanda hicho kinatengeneza pombe feki kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’.

Kufuatia tukio hilo, Naibu Waziri amesema kuwa Jeshi la Polisi inawashikilia watu wawili ambao ni wafanya kazi katika Kiwanda hicho huku mtu mmoja akisakwa na Jeshi hilo.

pombe-feki3

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Mashariki, Emmanuel Alphonce amesema kuwa Kiwanda hicho kimebainika baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani wa mwanamke huyo ambao wametilia shaka mwenendo wa biashara alizokuwa akizifanya.

pombe-feki pombe-feki1 pombe-feki4

La Galaxy Wamuweka Njia Panda Steven Gerrard
Argentina Yapoza Machungu, Yaitandika Colombia