Kiwanda cha kutengeneza maji na juice cha cha MO ENTERPRISES kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi kwa kosa la kumwaga maji machafu katika makazi ya watu, bila kupata kibali cha Baraza la taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC na kibali cha Bonde la wami ruvu, kinachoruhusu kuachia maji yaliyotibiwa kwenye mazingira.                                                                                                                                                                                                                                   Hayo yamebainika katika muendelezo wa oparesheni  ya ukaguzi wa mazingira na viwanda jijini Dar Es Salaam inayofanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina.

Kiwanda hicho kinatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni kumi kwa muda wa siku saba, pamoja na kufanya marekebisho ya miundominu kiwandani hapo na kupata kibali cha kutiririsha maji wanayoyatibu toka kiwandani hapo, kutoka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC.

Katika ziara Hiyo, NEMC pia imewatoza faini ya shilingi milioni tano kila moja wakazi tisa wa eneo la kiwalani Bam Bam kwa kile kinachodaiwa ni kutapisha maji ya vyoo katika mfereji mkubwa wa maji ya mvua maarufu kwa jina la mfereji wa Airport, Nakutakiwa kulipa faini hiyo ya jumla ya shilingi milioni arobaini na tano kwa muda wa wiki moja , kinyume na hapo watafikishwa mahakamani.

Aidha, Naibu Waziri Mpina pia alitembelea kiwanda cha Step Entertainment kinachotengengeza CD, tape na DVD na kujionea uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha maji ya chooni katika mazingira na kuwatoza faini ya shilingi milioni saba ambayo inatakiwa kulipwa ndani ya siku saba pamoja na kuwataka kuziba matoleo yote ya mifereji inayotoa maji machafu na kufanya usafi wa mazingira mara moja.

Timu hiyo ya Naibu Waziri Mpina pia ilitembelea kiwanda cha Royal na kukipa AMRI kali la kufanya kusafi wa mazingira katika mtaro wao kwa muda wa siku mbili

Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Morogoro, ukaguzi wa miradi ya maendeleo
Tundu Lissu aandika ujumbe akiwa mikononi mwa polisi baada ya kufanya mkutano