Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa faini ya shilingi milioni Thelathini kwa kosa la uchafuzi w a mazingira kwa kutiririsha maji taka na yenye sumu katika mto kibangu na kuhatarisha maisha ya mazingira na viumbe hai.

Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya kukagua viwanda nchini, sambamba na adhabu hiyo kiwanda hicho kimetakiwa kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo, pamoja kupeleka ripoti ya upimaji wa moshi na vumbi litokanalo na makaa ya mawe na maji yanayotoka kiwandani hapo ili serikali kujiridhisha kama si hatarishi kwa mazingira.

‘’Ili kujiridhisha NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji haya yanayotiririka ili tuone kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na kiwanda kiwasilishe cheti cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu Waziri Mpina.

Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho Bwana Mohamed Rajabu alipoulizwa kama ameikubali adhabu hiyo, alitupia lawama kwa NEMC na kusema kuwa wao ndo walitoa kibali cha athari ya tathimini ya mazingira kwa kiwanda hicho na ndiyo maana kinaendelea kufanya kazi na kuwa wangekuwa wanapita kwanza na kutoa onyo kwa wenye viwanda kabla ya kutoa adhabu kali ya mamilioni ya fedha.

Akihitimisha katika zoezi hilo Naibu waziri Mpina aliwataka wawekezaji na wenye viwanda nchini kutii sheria na kuthamini maisha ya wafanyakazi kwa kuyaweka mazingira safi na salama

Mke wa Lissu afunguka ya baada ya kumsikia mumewe akilia 'njaa' kituo cha Polisi
Kamanda Mpinga Azindua Mkakati Kukabiliana na Ajali Barabarani