Kiwanda cha kutengeneza kinywaji cha soda aina ya Pepsi kilichopo Kiwalani jijini jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni 25 na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku kumi na nne kwa kosa la uchafuzi wa mazingira, kwa kutiririsha maji machafu yenye kemikali katika mtaro wa maji ya mvua ya mtaa wa kiwalani.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa adhabu hiyo ya ukiukwaji wa sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kupitia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ya kukagua mazingira ya jiji la Dar es Salaam na mitaa ya viwanda.

Naibu Waziri Mpina alisema kuwa wawekezaji wenye viwanda wanapaswa kuelewa kuwa NEMC huwa inapita mara kwa mara na kutoa mwongozo, wa utekelezaji wa sheria ya mazingira na kuwataka wawekezaji waache dharau ya kuthaminisha maisha ya wananchi kwa gharama ndogo, na  kuwaasa wawe serious na sheria ya mazingira, na kuwaonya wamiliki wa kiwanda cha SBC Tanzania Limited. kuacha kabisa kutiririsha maji machafu, pamoja na kuelekeza kila kiwanda kiwe na Afisa Mazingira ambae ndiyo mshauri mkuu wa masuala ya mazingira.

Aidha Mhe. Mpina aliwataka wawekezaji pia wapeleke kwake malalamiko ya watendaji wa NEMC ambao wanaona hawawatendei haki.

Awali akitamka adhabu hiyo  Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Jaffari Chimgege alisema kuwa  pamoja na adhabu hiyo kiwanda hicho cha Pepsi pia kimekuwa na kosa la kutiririsha maji hayo machafu bila kuyatibu na kwa mujibu wa sheria ya wenye viwanda walitakiwa kukusanya taarifa ya ukaguzi kwa baraza, ili kuona kama wanatekeleza sheria ya mazingira na hawakufanya hivyo.

“Wafanyie kazi haraka taarifa ya ukaguzi.”

Kwa upande wake, Afisa Mauhusiano wa kiwanda hicho Bw. Alexandra Nyirenda aliliomba Baraza (NEMC) kuelekeza wenye viwanda zaidi ya mara mbili kabla ya kutoa adhabu, ili waweze kwenda sawa na  utekelezaji wa Sheria ya mazingira na kanuni zake kwani kujisahau ni ubinadamu.

Wakati huo huo; Mhe Naibu Waziri Mpina amezindua bomba lenye urefu wa kilometa mbili la, utoaji maji taka katika kiwanda cha bia cha Serengeti. (SBL) cha Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

TFF Yakanusha Kuvuja Kwa Ratiba, Yatangaza Ratiba Halali
Mke wa Trump azua jambo baada ya ‘ku-copy’ hotuba ya mke wa Obama