Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Nassredine Nabi amemwagia sifa Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephen Aziz Ki, kufuatia kuendelea kuonyesha uwajibikaji kwenye kikosi chake.

Aziz Ki alisajiliwa Young Africans miezi miwili iliyopita akitokea kwa Mabingwa wa Soka nchini Ivory Coast ‘Asec Mimosas’ ambayo msimu uliopita ilicheza dhidi ya Simba SC, Hatua ya Makundi kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho.

Nabi amesema Kikosi chake kimeanza kula matunda ya Aziz Ki baada ya kufunga katika michezo miwili mfululizo, akifunga dhidi ya Mtibwa Sugar na baadae dhidi ya Zalan FC kutoka Sudan Kusini.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema anafurahishwa na kiwango cha nyota huyo ambacho kinaendelea kudhihirisha thamani ya ubora wake kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa.

“Aziz Ki ni mchezaji mzuri, ninarudia tena kusema hilo, ambacho kipo kwa upande wake pia hutokea kwa wachezaji wengi wageni ndani ya timu na ndio maana utaona kadri siku zinavyozidi kusogea mbele basi mchezaji huyu anazidi kuyazoea mazingira na kuonyesha kiwango kizuri.

“Unajua ukiwa Kocha, jambo ambalo huwa sio nzuri ni kuzungumzia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, hivyo pengine ukiizungumzia timu kwa ujumla basi inakuwa na afya zaidi jambo ambalo kitimu Aziz Ki bado ana mchango mzuri kwa wenzake na tunategemea makubwa kutoka kwake. amesema kocha Nabi.

Akpan awatoa wasiwasi Mashabiki Simba SC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 20, 2022