Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa kwa miaka 60 ya uhuru ikiwepo kupungua kwa umasikini.

Rais Samia amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Taasisi za fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ukumbi wa Jakaya Kikwete leo Novemba 25, 2021.

“Tumepunguza kiwango cha umasikini kutoka asilimia 28.6 mwaka 2015 hadi asilimia 26 mwaka 2020, ni hatua kubwa” amesema Rais Samia.

Rais Samia pia amesema kiwango cha Uhai kimeongezeka kutoka miaka 50 hadi miaka 66 kwa sasa kwa sababu hali ya maisha inazidi kuwa bora.

Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha Nchini una lengo la kupitia na kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.

Rais Samia: Riba za mikopo benki zitashuka zaidi
Rada za Kocha Pablo zainasa Red Arrows