Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Tixon Nzunda amesema kuwa, kiwango cha watumiaji wa bangi kinazidi kuongezeka nchini, hivyo ipo haja ya kufanyika jitihada kukabiliana na hali hiyo.

Amesema hayo baada ya kutembelea makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA),amesema kuna kila sababu ya kuongeza vita dhidi ya walimaji, wasambazaji na watumiaji wa bangi.

“Tumefanikiwa kudhibiti hizi cocaine na heroin kuingia nchini, changamoto inabaki kwenye bangi, watumiaji wanazidi kuongezeka”amesema Nzunda

“Niwaombe wananchi na Watanzania kwa jumla kutangaza vita dhidi ya walimaji, wasambazaji na watumiaji wa bangi. Tunusuru kizazi chetu,” amesema Nzunda.

Nzunda amesema Serikali ipo makini kuhakikisha haitamuacha mtu yeyote anayejihusisha na biashara hiyo haramu.

Naye Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya amesema jitihada kubwa zimeendelea kufanyika ili kukabiliana na bangi, ikiwamo kuyabaini mashamba na kuyateketeza.

RC Makalla atoa maagizo kuhusu 'Corona'
PICHA: Mabingwa ASFC wawasili Dar es salaam