Watu watatu wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora wakikabiliwa na mashitaka mawili ya mauaji kufuatia tukio la kumzalisha mwanamke mjamzito bila kuwa na taaluma ya kuzalisha ambaye alikuwa na ujauzito wa watoto mapacha na kupelekea kifo chake.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kijiji cha Miswaki wilayani Uyui mkoani Tabora ambapo watuhumiwa hao ni Ezekiel Kazimoto, Victoria Makomba na Regina Balaye wote wakiwa wanafanya kazi ya kuuza dawa za binadamu katika maduka ya dawa baridi.

Akisoma maelezo ya kosa mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora Jovith Kato wakili upande wa Jamhuri, Juma Masanja alisema watuhumiwa hao wote watatu wanadaiwa kutenda makosa mawili.

Kosa la kwanza ni kumuua Ester Chamika ambaye alikuwa mjamzito wakati walipokuwa wakimzalisha huku wakitambua kwamba hawana ujuzi wa kufanya hivyo na kumsababishia kifo.

Muigizaji wa ‘Star Wars’ afariki dunia kwa Corona
Wananchi Mauritius kununua bidhaa kwa Alphabet

Comments

comments