Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Kizz Daniel ameomba radhi kwa mashabiki wake wa Tanzania kwa kutohudhuria kwenye onesho lililokuwa limeandaliwa lifanyike mwishoni mwa juma lililopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kizz ameeleza sababu kadhaa zilizochangia kushindwa kutokea mpaka kupelekea kuzuka kwa ghasia iliyotokana na mashabiki kupata ghadhabu.

“Nilipofika Nairobi toka Kampala ndege niliyotakiwa kuunganisha nayo nilikuta imeshaondoka, nilikaa Nairobi kwa masaa nane, nikapata ndege ya kuunganisha saa mbili na nusu usiku, nilipofika Dar tukagundua kuna vitu vyangu vimesahaulika, wakasema watanitumia,” alisema Kizz.

Kizz ameongeza kuwa waandaaji walimuhakikishia watapata vifaa vingine na akawa tayari kutumbuiza ila alipofika ukumbini muda ulikuwa umweisha.

“Waandaaji wakanihakikishia tutapata vifaa vingine, tukafika hotelini saa saba usiku nikaituma band yangu kwenda ukumbini kufanya mazoezi, bahati mbaya bendi ikashindwa kwa sababu mashabiki walishaingia ukumbini,” aliongeza.

“Nilijaribu kuwasiliana na wabunifu wa mavazi wa hapa ili kupata nguo, nilipoamua kutoka kwenda ukumbini niliambiwa sio salama tayari Mashabiki walipata hasira,”

“Tukakubaliana na Waandaji kwamba tutaomba radhi kwa Mashabiki na tutaandaa show nyingine, siku ya pili taarifa zikawa zimesambaa na Polisi wakanifuata Hotelini, sio kunikamata ila kunihoji kwa kilichotokea.”  Amesema Kizz Daniel. 

Kizz Daniel alikuja Tanzania kwa jailli ya kufanya onesho liliondaliwa na Kampuni ya uandaaji wa matamasha ya Muziki ya Sraight Up siku ya Jumapili, Next Door Arena lakini hakuweza kupanda jukwaani na kuleta ghadhabu kwa mashabiki.

Mbunge mbaroni kwa kumshambulia mpiga kura.
Shambulio lauwa Wanajeshi 17 na raia wanne