Mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba wataanza na Mbabane Swallows Swaziland katika Mzunguuko wa Awali wa mchujo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 20158/19.

Mabingwa hao wenye maskani yao makuu mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam, endapo watafanikiwa kuvuka katika mzunguuko huo watakwenda hatua ya kwenye mzunguuko wa mwisho, kabla ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Katika mzunguuko wa pili Simba huend ikamenyana na mshindi kati ya Uniao Desportiva Do Songo ya Msumbiji na Nkana FC ya Zambia, anayochezea beki Mtanzania, Hassan Kessy.

Nao mabingwa wa soka wa Zanzibar, Maafande wa JKU wamepangwa kukutana na Al Hilal ya Sudan na mshindi atakaepatikana atamenyana na mshindi kati ya APR FC ya Rwanda na Club Africain ya Tunisia.

Michezo ya mzunguuko wa awali itachezwa kati ya Novemba 27 na 28 na marudiano Desemba 4 na 5, mwaka huu, wakati michezo ya kwanza ya mzunguuko wa pili itachezwa kati ya Desemba 14 na 16 na marudiano Desemba 21 na 23, mwaka huu.

Katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF), Mtibwa Sugar wataanza na Northern Dynamo ya visiwa vya Shelisheli na wakfanikiwa kushinda watakutana na timu ya Mamlaka ya jiji La Kampala  K.C.C.A ya Uganda.

Wawakilishi wa Zanzibar, Zimamoto wamepangiwa kukutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na mshindi atakaepatikana katika mchezo huo atakutana na mshindi mchezo kati ya El Geco ya Madagascar na Deportivo Unidad ya Equatorial Guinea.

Ujerumani yatonesha kidonda cha Wayahudi
Wanunuzi wa Korosho sasa kufutiwa leseni, wapewa siku nne

Comments

comments