Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2017. Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Tarehe 24- 29/04/2017,  viwanja vya wazi vya Tanganyika packers, Kawe Jijini Dar es salaam.

Mashindano hayo yatatanguliwa na Mkutano Mkuu wa wanachama wa (BFT) wenye  lengo la kupitisha rasmu ya Katiba.

Ratiba ya mashindano hayo itakuwa kama ifuatavyo:-

  • Tarehe 24/04/2017 Saa 2.00 Asubuhi Hadi Saa 6.00  Mchana katika ukumbi wa Masai Garden Kawe utafanyika Mkutano mkuu wa BFT ajenda ikiwa kupitisha  rasmu ya Katiba
  • Tarehe 25/04/2017 Saa 2.00 – 4.00 Asubuhi zoezi la kupima uzito na afya kwa mabondia wote watakaoshiriki mashindano hayo wanawake na wanaume upimaji huo utafanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, Saa 5.00- 6.00 Mchana , kutayarisha ratiba ya mashindano , na Saa 9.00Alasiri ufunguzi na mashindano kuanza hatua ya mtoano wa kwanza.
  • Tarehe 26/04/2017 Saa 2.00- 00 Asubuhi, kupima uzito na Afya. Saa 8.00 Mchana mashindano  kuendelea hatua ya mtoano wa pili
  • Tarehe 27/04/2017 Saa 2.00- 3.00 Asubuhi kupima uzito na afya kwa mabondia wote walioingia robo fainali, Saa 8.00 Mchana mashindano kuendelea hatua ya Robo fainali.
  • Tarehe 28/04/2017 Saa 2.00 – 3.00 Asubuhi kupima uzito na afya kwa mabondia wote walioingia nusu fainali, Saa 8.00 Mchana Mashindano kuendelea hatua ya Nusu fainali
  • Tarehe 29/04/2017 Saa 2.00 – 3.00 Asubuhi kupima uzito na afya kwa mabondia wote walioingia Fainali, Saa 8.00 Mchana Mashindano kuendelea hatua ya fainali na baadae kufunga mashindano rasmi.
  • Tarehe 30/04/2017 timu zote kuondoka.

Timu ambazo hadi leo zimedhibitisha  kushiriki ni Ngome, JKT, Polisi, Magereza, Temeke, Morogoro, Dodoma, Tabora , Kigoma, Tanga na Mwanza.

Waamuzi walioteuliwa kuchezesha mashindano hayo ni Mohamed Kasilamatwi. Riadha Kimweri, Maneno Omari, Mohamed Rashid, Marco Mwankenja, Joseph Kapandila na Mafuru Mafuru.  Daktari wakati wote wa mashindano atakuwa ni Mussa Maira.

Video: Sakata la Richmond laibuka upya, Uhai wa Ben Saanane utata
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 21, 2017