Bilionea wa Urusi, Alisher Usmanov amewasilisha ombi la pauni bilion moja kuinunua Arsenal kutoka kwa mmiliki wake Stan Kroenke kwa ajili ya kuiwezesha kupata mafaniko hasa kutwaa mataji mbalimbali.

Gazeti la The Financial Times limeripoti kuwa Usmanov aliwasilisha ombi hilo mwezi uliopita na kwamba Kroenke hajatoa tamko ramsi kuhusu ombi hilo la mfanyibiashara huyo wa vyuma huku akimiliki  asilimia 30 ya hisa za Arsenal.

Hata hivyo pamoja na kumiLIki hisa hizo mfanyabiashara huyo bado hana mamlaka yeyote ya kutoa maamuzi katika Klabu hiyo ya Arsenal huku wadau mbalimbali wa Klabu hiyo wakitaka akabidhiwe timu.

Usmanov amesema kuwa kwa vyovyote vile Kroenke ndiye mwenye kubeba lawama zote kwakuwa yeye ndiye aliyesababisha hayo yote yanayotokea ndani ya Arsenal kwa kukuwa na mipango butu isiyokuwa na mitizamo chanya.

 

Korea ya Kaskazini yafanya jaribio lingine
Video: Serikali imepiga hatua kubwa katika uwekezaji-Mwijage