Chama cha soka nchini England (FA), huenda kikakubali kuuza uwanja wa Wembley kwa mmiliki wa klabu ya Fulham Shahid Khan.

Mtendaji mkuu wa FA Martin Glenn, amenukuliwa na magazeti The Sun na Evening Standard akieleza mpango huo, ambao utakua na makubaliano maalum kabla ya kuuzwa kwa uwanja huo mkubwa kuliko viwanja vyote nchini England.

Kwa sasa uwanja wa Wembley unatumiwa na klabu ya Tottenham Hotspur kama uwanja wao wa nyumbani, baada ya kuingia makubaliano maalum na FA mwanzoni mwa msimu wa 2017/18, kufuatia uwanja wao wa White Hart Lane kuwa katika maboresho ya ujenzi.

Tajiri Khan ambaye pia anamiliki klabu ya Jacksonville Jaguars inayoshiriki michuano ya Amerikan Football (NFL) nchini Marekani, amejipanga kununua uwanja wa Wembley kwa Pauni milioni 100.

Uwanja wa Wembley ambao kwa sasa una mandhari ya kipekee duniani, ulivunjwa mwaka 2003, na kujengwa upya hadi mwaka 2007 ambapo ulianza kutumika tena.

Gharama zilizotumika katika ujenzi wa uwanja huo kwa mara ya pili zinakadiriwa kufiki Pauni milioni 800.

Jerome Boateng kusubiri kombe la dunia
Watu 9 wakamatwa wakiandamana Posta, Dar es Salaam