Klabu ya Simba na waashindi wa Kombe la FA, siku ya jumanne inatarajia kutimkia nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao ambapo inamatarajio makubwa ya kufanya vizuri.

Simba imejizatiti kufanya vizuri kwenye msimu mpya, hivyo imepanga kuwa na maandalizi ya maana nchini humo na itarejea nchini siku chache kabla ya maadhimisho ya Simba Day, Agosti 8 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, imesema kuwa Simba ikiwa Afrika Kusini itacheza mechi za kirafiki ili kocha wake, Joseph Omog aweze kuona upungufu uliopo na kuufanyia kazi.

Hata hivyo, Klabu hiyo ambayo ni bingwa wa kombe la FA imepita misimu kadhaa haijachukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara imetamba kuwa imefanya usajili mzuri kwa kipindi hiki

Video: DataVision, TAFCA kuwakomboa wasanii wa sanaa za mikono
JPM atuma salamu za rambirambi kwa Dkt. Mwakyembe

Comments

comments