Klabu za ligi kuu ya England, zimeripotiwa kuomba kutumia wachezaji wa akiba watano badala ya watatu, kama EPL itarejea kumalizia mechi zilizosalia msimu huu wa 2019-20.

Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, mapendekezo hayo yametolewa na klabu za EPL baada ya kujadiliana namna nzuri ya kumaliza msimu bila kuwaathiri wachezaji.

Kumekuwepo na majadiliano ya EPL kurejea mwezi Mei na kumalizika mwezi Juni, huku wengine wakipendekeza mechi kuchezwa mfululizo.

Wakati ratiba hiyo huenda ikawa burudani kwa mashabiki, kwa wachezaji inaweza kuwa na athari mbaya hususani kupata majeraha.

Vilevile, kuna ripoti kwamba, imependekezwa VAR nayo itolewa katika mechi zilizosalia ili kuepusha watu kuambukizana virusi vya Corona.

Teknolojia ya VAR, inawataka watu wakae chumba maalumu kufanya marejeo ya matukio ya uwanjani, jambo linalohofiwa kwamba linaweza kusababisha mlipuko wa Corona.

Video: Gongo ruksa, Wapinzani wang'aka hotuba kuzuiwa
EPL yapigwa tena kalenda

Comments

comments