Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amewakataza wachezaji wake kushika nembo ya klabu hiyo iliyopo katika sehemu ya korido ya kuelekea uwanjani ukitokea katika vyumba vya kubadilishia.

Klopp amevunja utamaduni huo kwa wachezaji ambao ulikua umezoeleka tangu enzi na enzi ambapo ilifikia hatua hata mameneja waliomtangulia walikua wakiigusa nembo hiyo.

Klopp amechukua maamuzi ya kuwakata wachezaji wa Liverpool kutofanya hivyo kwa kuamini nembo ya klabu ni kitu kikubwa na kinapaswa kuheshimiwa kama ilivyo kwa vitu vingine ambavyo havishikwi hovyo hovyo.

Hata hivyo Klopp amewapa masharti wachezaji wake kushika nembo hiyo, endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano yoyote watakayoshiriki katika kipindi chote ambacho atakuwepo klabuni hapo.

“Nimewakataza wachezaji wangu kushika nembo ya klabu inayoonekana pale koridoni, ili kuipa heshima ya kipekee, na watakua huru kuishika endapo watafanikiwa kurejesha fadhila ya kutwaa ubingwa wa michuano yoyote katika kipindi nitakachodumu Anfield.” Amesema Klopp

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani alifichua siri hiyo baada ya ushindi wa mabao maanne kwa matatu walioupata usiku wa kuamkia hii leo katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa league dhidi ya Borussia Dortmund.

Takukuru kumrudisha kizimbani Mhando wa Tanesco
Kinnah Phiri: Sasa Tuko Kwenye Kiwango Kizuri