Kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) kitaondoka jijini Dar es salaam leo jioni (Desemba 30), kuelekea Jijini Mbeya, tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Januari mbili katika uwanja wa Kumbukumbu ya  Sokoine.

KMC FC itacheza mchezo huo, huku ikikumbuka matokeo ya furaha waliyoyapata kwenye mchezo mzunguuko wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam, ambapo Mbeya City walikubali kufungwa mabao manne kwa sifuri kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa KMC FC Christina Mwagala amesema, wachezaji wote wanaotarajia kuanza safari ya kuelekea jijini Mbeya wapo katika hali nzuri na wote kwa ujumla wana morari ya kupambana na kupata matokeo mazuri, yatakayowapa alama tatu muhimu ugenini.

Mapema hii leo kikosi cha KMC FC kilifanya mazoezi yake ya mwisho kikiwa jijini Dar es salaam, ikiwa ni katika mkakati wa kujiweka vizuri kuelekea kwenye mchezo huo.

KMC FC ipo kwenye nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 21, huku wapinzani wao Mbeya City wakishika nafasi ya 16 kwa kufikisha alama 13.

Isco kuhamia England, Wijnaldum kutimkia La Liga
Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni wampeleka jela miaka 3