Timu ya Manispaa ya Kinondoni ‘KMC FC’ kesho Jumatano (Novemba 23) itashuka katika Dimba la Liti Mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa majira ya saa nane mchana.

Kikosi cha KMC FC kimeshawasili mjini Singida tangu jana Jumatano (Novemba 21) na leo Jumanne (Novemba 22) kitafanya mazoezi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa KMC FC Christina Mwagala amesema mbali na maandalizi ya wachezaji, maandalizi mengine ya mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars yameshakamilika.

“Tumefika jana Jumatatu mjini Singida salama, tunamshukuru Mungu safari yetu ilikuwa nzuri, tunawaheshimu Singida Big stars kwa kuwa inawachezaji wazuri, Benchi la ufundi zuri, lakini hata KMC FC tunawachezaji wazuri na wenye ubora mkubwa ambao wanaweza kupambana sehemu yoyote na kupata matokeo.”

“Tunafahamu kiu ya mashabiki zetu kuwa wanahitaji matokeo mazuri, na sisi tunawaahidi kuwa siku zote Timu bora huwa haipotezi mchezo mara mbili, hivyo wachezaji wetu wanahari na morali nzuri ,tuzidi kuwasapoti kila mchezo wanapokuwa uwanjani.” amesema Mwagala

Katika mchezo wa kesho Jumatano (Novemba 23), KMC FC itawakosa wachezaji watatu ambao ni Awesu Ally Awesu, Emmanuel Mvuyekure pamoja na Kelvini Kijili ambao ni majeraha.

UNRSF yalia na ajali za barabarani kwa watoto
Wataalamu wataka ushirikiano kuikabili TB