Kocha msaidizi wa Timu ya KMC FC, Habibu Kondo amesema kuwa hadi sasa kikosi chake kipovizuri kuelekea mpambano wa kesho dhidi ya JKT Tanzania mchezo utakaopigwa katika Dimba la Jamuhuri Jijini Dodoma saa 8.00 mchana.

Ameongeza kuwa licha ya kwamba ametoka kupoteza michezo mitatu mfululizo, lakini hivi sasa anachokiangalia ni mchezo wa kesho na kwamba kikosi hicho cha wana Kino Boys, kipo katika hali nzuri na kwamba wanauwezo mkubwa wakushinda mchezo huo licha ya kwamba watakuwa ugenini.

Kocha Habibu amesema kuwa mchezo wa kesho ni mwingine na kwamba anachokiangalia ni kuweka sawa mipango na wachezaji wake katika kuhakikisha kuwa anapata matokeo mazuri ikiwa ni kuchukua alama tatu dhidi ya wapinzani wake.

“Tunakwenda kucheza na Timu Ngumu, tunaiheshimu JKT Tanzania, lakini niseme kwamba kesho KMC FC ndio itakayokuwa ngumu na bora kwao hatuangalii tumepoteza michezo mingapi ila tuna angalia kesho tunapataje matokeo tukiwa ugenini hapa Jamuhuri Dodoma” amesema Kocha Habibu.

Hata hivyo Habibu amesema kuwa katika kikosi chake atawakosa wachezaji wanne kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambao ni Hassan Kabunda, Abdul Hillary, Hassan Kapalata pamoja na Reliant Lusajo.

Serikali kurasimisha taarifa za wananchi
Wachezaji FC Platnum wazuiwa kutumia simu