Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC (Kino Boys) leo Al-Khamis imeanza safari ya kuelekea Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kucheza mchezo wa mzunguuko wa watatu wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani humo.

KMC FC inakwenda kucheza mchezo wake wa kwanza ugenini, huku ikiwa imejizatiti inafanya vizuri katika mchezo huo, kama ilivyokuwa katika michezo miwili iliyopigwa katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ambayo hivi sasa inaongoza ligi, mbali na mchezo huo wa  Mwadui FC  lakini pia itacheza mchezo mwingine na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera Septemba 25 mwaka huu.

Katika msafara huo, KMC FC imeondoka na wachezaji 22 huku wachezaji sita wakiachwa akiwemo Sadalla Mohamed Lipangile ambaye ni majeruhi, lakini Afya yake inaendelea kuimarika vizuri.

KMC FC itacheza dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Mwadui Complex na kwamba inatarajia kuwasili mkoani humo Septemba 19 na na hivyo  itapumzika kabla ya kuanza kwa mazoezi mengine ya kujiweka tayari dhidi ya mchezo huo.

Katika michezo yake miwili ya nyumba, KMC FC ilifanya vizuri kwa kuanza kumfunga Mbeya City Magoli manne kwa sifuri, Tanzania Prisons magoli mawili kwa moja na hivyo kuiwezesha kusalia katika fanasi ya kwanza Ligi Kuu Tanzania bara.

PICHA - LIGUE 1 yapitisha msumeno wa adhabu
Zaidi ya wafungwa 200 watoroka