Ikiwa maelfu ya watu wanajipanga kuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant na bintiye Gigi Bryant, hatimaye mke wake Vanessa Bryant aweka wazi mahala patakapo fanyika shughuli hiyo.

Vanessa ameweka posta (tangazo) pichani kwenye ukurasa wake wa instagram likiwa na taarifa ya siku na mahali patakapo tumika kufanya ukumbusho wa maisha wa mwili wa marehemu mumewe na binti yake ambapo itakuwa ni siku ya Jumatatu, Februari 24 katika ukumbi wa ‘Staples Center’.

Imeteuliwa siku anayoagwa Kobe na Gigi kuwa ni Februari 24 kutokana na umuhimu wa namba ya jezi walizokuwa wakizivaa.

Kobe alikuwa akivaa jezi namba (24) na Gigi alivaa jezi namba (2). Pia ukumbi wa ‘Staples Center’ umeteuliwa kwa sababu ndiyo ukumbi aliocheza kikapu Kobe Bryant maisha yake yote katika mchezo huo.

Hata hivyo tuzo za Oscar’s zitakazo fanyika Jumapili hii huko Los Angeles Marekani wanatarajia kumpatia marehemu Kobe tuzo ya heshima.

Kwa mujibu wa mtandao wa Entertainment Tonight waandaaji wa tuzo hizo wameuthibitishia mtandao huo kuwa nguli huyo wa kikapu Duniani atapewa heshima katika kipengele maalumu kwa ajili ya kumbukumbu.

 

Maafisa wa Jeshi 26 washindwa kumaliza mafunzo, 128 watunukiwa kamisheni na Rais
Mwamposa apumzishwa, kanisa kuendelea na mafuta ya upako

Comments

comments