Kaimu Kocha Mkuu wa Coastal Union Joseph Lazaro amewatuliza mashabiki wa klabu hiyo, kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi chao kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Coastal Union mwishoni mwa juma lililopita ilicheza mchezo wake wa 21 wa Ligi hiyo dhidi ya Kagera Sugar iliyokua nyumbani Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba-Kagera na kuambulia sare ya 0-0, kabla ya kupoteza dhidi ya Geita Gold FC jana Jumanne (Januari 24) kwa 1-0.

Kocha Lazaro amabye ameachiwa mikoba ya kuingoza kwa muda Coastal Union baada ya kuondoka kwa Kocha kutoka Kenya Yusuph Chipo, amesema anaamini kikosi chake kinapita wakati mgumu, lakini muda si mrefu mambo yatawanyookea.

Amesema hali hiyo inatokana na maingizo ya wachezaji sita waliosajiliwa wakati wa Dirisha Dogo la Usajili, hivyo wanahitaji kuingia kwenye mfumo wa timu ili kuzoeana na wachezaji waliowakuta ili kupata timu imara.

“Kwa kweli hatuna mwenendo mzuri kwenye Ligi Kuu kiasi kwamba hata kupata alama moja tunaona kama almasi.”

“Timu inahotaji muda, tumesajili wachezaji sita ambao wanahitaji muda ili kuingia kwenye mfumo, lakini nafikiri baada ya hapo timu itaanza kufanya vizuri kwenye michezo inayofuata.

Wachezaji waliosajiliwa Coastal Union kupitia Usajili wa Dirisha Dogo ni Ndikumana Justin (Burundi), Felly Mulumba (DR Congo), Geolord Mwamba (Kenya), Enock Jiah, Omar Banda na Yusuph Athuman (Tanzania).

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Coastal Union inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama 19, zilizotokana na kushinda michezo minne, sare saba na imepoteza kumi.

Mwana FA ateta na Madiwani Sheria umiliki ardhi Utawala bora
Tanzania Prisons: Odhiambo hajafukuzwa