Kocha Mkuu wa Taifa ya Gabon amemruhusu mshambuliaji wake, Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka kwenye michuano ya Afcon na kurudi klabuni kwake ili aende akajiuguze baada ya kupata maambukizi ya Corona.

Kocha Patrice Neveu pia amemruhusu kiungo anayecheza Ufaransa, Mario Lemina ambaye karudi kwenye timu yake ya Nice ambapo hakuweza kucheza hata dakika moja kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Cameroon.

“Tumefanya maamuzi sahihi kuwarudisha kwenye klabu zao, wanaweza kuangaliwa vizuri wakiwa kule,” amesema kocha Neveu akiwaambia waandishi wa habari.

Mchezaji huyo hajafanikiwa kucheza mchezo wowote kwenye michuano hiyo, ambapo kwa sasa inaelekea hatua ya mtoano kuelekea Robo Fainali, Nusu Fainali na Fainali.

Ahmed Ally: Lwanga amenusurika Simba SC
Uongozi Simba SC kumuweka chini John Bocco