Baada ya kuichakaza Jwaneng Galaxy nyumbani kwao Botswana, Kocha wa Mabingwa Tanzania Bara na Wawakilishi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Simba SC, Didier Gomes, amefichua siri ya mbinu alizotumia kushinda ugenini jana Jumapili (Oktoba 17).

Simba SC ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0, yaliyofungwa na Nahodha na Mashambuliaji John Raphael Bocco dakika ya 02 na 05 kipindicha kwanza.

Gomes amesema katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hasa za ugenini unatakiwa kucheza kwa nidhamu kuhakikisha hufungwi bao na kutumia nafasi zinazopatikana ili kujiweka sehemu salama kuelekea mechi ya marudiano.

Gomes amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya na kujitahidi kufuata maelekezo walioyowapa na kusababisha kupatikana kwa ushindi huo umuhimu.

“Unapocheza ugenini siyo lazima kucheza soka la kuvutia badala yake unatakiwa kucheza kwa nidhamu ya kujilinda na kutumia nafasi unazopata kama wachezaji wangu walichofanya leo, nawapongeza sana kwa hilo,” amesema Gomes.

Akizungumzia mabao mawili ya haraka tuliyofunga, Gomes amesema ni jambo ambalo tumelifanyia kazi mazoezini na wachezaji wameenda kulikamilisha uwanjani.

“Tuliwatazama Galaxy kupitia mkanda wa video tukawaona wana shida kwenye mipira kona na ya kutenga hivyo tukatumia mapungufu yao kupata mabao,” amesema Gomes.

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Jumapili (Oktoba 24), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Biashara United waishukuru TFF, TPLB
Ethiopia yakataa chakula