Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Didier Gomes Da Rosa amewapongeza wachezaji wake kwa kutekeleza maelekezo anayowapa katika michezo ya ushindani na wanapokuwa mazoezini.

Gomez ametoa pongezo hizo, huku kikosi chake kikiwa safarini kuelekea nchini Misri kupitia Dubai, tayari kwa mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi dhidi ya Al Ahly, utakaounguruma Ijumaa (April 09).

Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa amesema nidhamu ya kufuata maelekezo kwa wachezji wake imekua njia sahihi iliyowafikisha kwenye furaha ya kutinga hatua ya Robo Fainali, wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Gomes amesema: “Kila mchezaji wangu amekua na nidhamu kubwa ya kufuata maelekezo tukiwa mazoezini na kwenye michezo ya mashindano, hii imekua silaha yetu kubwa ya kufanikisha tuliojiwekea tulipoanza kucheza hatua ya makundi.”

“Kikubwa ambacho tulikuwa tumepanga ni kufuzu na kuongoza kundi na yote tumefanikiwa. tunaenda kucheza mchezo wetu wa mwisho ugenini na baada ya hapo tutaanza maandalizi ya kutosha ya mchezo wa robo fainali.”

Kikosi cha Simba SC kimeondoka nchini leo Jumanne (April 06) majira ya saa 9:25 alasiri kwenda nchini Misri kupitia Dubai.

Msafara wa kikosi hicho umeondoka na jumla ya wachezaji 25 ambapo utapumzika Dubai na kesho Jumatano (April 07) asubuhi utaondoka kwenda Cairo, Misri na kufika saa 4:05 asubuhi.

Simba inaenda Cairo Misri kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya wenyeji wao klabu ya Al Ahly ya Misri mchezo ambao utachezwa Ijumaa ya (April 09).

Simba SC inaongoza msimamo wa ‘Kundi A’ ikiwa na alama 13, ikfuatiwa na Al Ahly yenye alama 08, huku AS Vita ikishika nafasi ya pili na Al Merrikh inaburuza mka kwa kuwa na alama 02.

Simba SC na Al Ahly zimeshafuzu hatua ya Robo fainali, hivyo mchezo wao wa Ijuma (April 09) utakua ni wa kukamilisha ratiba ya michezo ya ‘Kundi A’.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 7, 2021
NEC yatupilia mbali pingamizi CCM dhidi ya ACT- Wazalendo